KAGERE, OKWI WAJIFUA NA KIKOSI CHA SIMBA LEO, WAWILI WAKOSEKANA
Straika hatari wawili wa klabu ya Simba, Meddie Kagere na Emmanuel Okwi wameungana na wenzao leo kujifua kwenye Uwanja wa Boko Veterani kwa ajili ya maandalizi ya mechi za Ligi Kuu Bara.
Simba wanaendelea na mazoezi kwenye Uwanja huo wakijiandaa na mchezo dhidi ya Ndanda FC utkaopigwa mjini Mtwara Jumamosi ya wiki hii.
Kagere aliyekuwa Uganda kwa majukumu ya timu ya taifa na Kagere aliyekuwa Rwanda, wote wametua rasmi leo mazoezini na kuonesha moto uleule wa siku ziku zote.
Licha ya wawili hao kuanza mazoezi, wachezaji wengine wa timu hiyo Mrwanda Haruna Niyonzima na Juuko Murushid hawajaonekana huku sababu za wao zikiwa hazijulikani.
Murushid na Niyonzima hawajaonekana ndani ya dimba tangu pazia la michuano ya Ligi Kuu Bara msimu huu lifunguliwe Agosti 22 2018.
0 COMMENTS:
Post a Comment