Kiungo wa zamani wa Simba na Taifa Stars, Amri Kiemba ameweka wazi kuwa wachezaji wanaocheza nje na Tanzania wataisaidia sana Taifa Stars katika mbio za kusaka nafasi ya kucheza Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon).
Kiemba ambaye ameichezea Stars kwa miaka kadhaa akimudu vyema kucheza nafasi ya kiungo mshambuliaji kabla ya kuamua kustaafu kucheza.
Kiemba amesema ongezeko la wachezaji wengi wanaocheza nje ya Tanzania kunazidi kuongeza chachu katika timu ya taifa, kwani wachezaji huleta vitu vipya.
"Akina Msuva na wenzake kama Samatta na wachezaji wote wanaocheza soka la kimataifa wataisadia sana timu yetu ya Taifa, kwani wanavyocheza nje wanakutana na changamoto pamoja na mbinu mpya ambazo kimsingi huwa zinasaidia sana," alisema Kiemba.
0 COMMENTS:
Post a Comment