September 3, 2018




Rais wa TFF, Wallace Karia na Katibu wake mkuu, Wilfred Kidau leo walihudhuria mazoezi ya kikosi cha Taifa Srars kinachojiandaa na mechi dhidi ya Uganda.

Taifa Stars ilikuwa ikifanya mazoezi kwenye Uwanja wa Boko Veterani na Karia na Kidau walikuwa kati ya walioshuhudia mazoezi hayo.



Kocha wa Taifa Stars, Emmanuel Amunike ameendelea kukifua kikosi chaka kujiandaa kuwavaa Waganda Jumamosi.

Taifa Stars ina kibarua kigumu ugenini dhidi ya Waganda watakaoongozwa na Emmanuel Okwi ambaye ni mshambuliaji wa Simba.


Karia alikuwa akifuatilia kwa ukaribus sambamba na Kidau wakati kocha huyo Mnigeria akifanya kazi yake.

3 COMMENTS:

  1. Hao ndio hawana maana kabisa. Siku tatu kutoka kwenye kanuni za FIFA mchezaji anatakiwa kujiunga na timu ya Taifa. Wachezaji waliondolewa Taifa wa Simba ni wachezaji muhimili wa taifa stars uliojengwa na makocha waliopita kwa muda mrefu. Ni wachezaji wenye uzoefu wa mechi za kimataifa. Ni wachezaji wanofundishwa na miongoni mwa walimu bora nchini kwenye timu yao. Ni wachezaji wanaohitaji maelekezo sio kufundishwa kutoka kwa kocha yaani ni maprofossional. Kama wao TTF kwa kutumia nguvu na mabavu na kuona wachezaji hao si chochote si lolote basi Taifa Stars wataisoma namba baada ya mechi ya Kampala. Kilikuwa kitendo cha dharau kwa TTF na kama Amunike kashiriki kuwatimuwa wale wachezaji wa Taifa, tuwache kuwaita wachezaji wa Simba ni wachezaji wa Taifa.kwani kimsimgi na kanuni hawakuwa na kosa walilofanya hadi kuondolewa timu ya Taifa ni maamuzi ya hovyo kana kama viongozi wa TTF wamepokea mrungura kutoka Uganda ili waihujumu Taifa Stars.

    ReplyDelete
  2. Hao wachezaji wako wangecheza wap tuna maproo kumi Mzee baba acha wakimataifa watubebe hapo nambolee

    ReplyDelete
  3. Swift revenge ends in bitter end. Kosa la kwanza haliwachi mke. Nguzo sita zilizofukuzwa zilikuwa nguzo madhubuti kuihami nyumba kutokana hata na Sunami iliyotesa kwwinhi duniani na kilichotakiwa ni busara wala sio kutimuwa na ingekuwa di busara basi leo yanga ingekuwa bila ya wachezsji. Kuwepo kwa hiyo miamba sita kungewafanya wapinzsni wajione hawana lao tangu mwanzo. Kutokana na Kocha Amoniko mpendwa mwenye uwezo wa hali yajuu
    Kisoka ilibifi ashauriwe tu na wala si kupingwa lakini badala yake aliungwa mkono mojakwamoja. Hata hivo tunamuombea kocha huyo kila la heri kstika mtihani wake wa kwanza na pindi hakufanikiwa iwe funzo tosha kwa wale waliomuelekeza au kumuunga mkono kwa hatua hiyo iliyolalamikiwa na wengi n

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic