September 11, 2018




Gwiji la soka kutoka Argentina, Diego Maradona ameamua kurejea tena katika soka na kuwa kocha.

Ametambulishwa katika timu inayoshiriki daraja la kwanza ya Dorados of iliyo katika mii wa Sinaloa nchini Mexico. Tayari uteuzi wake umezua gumzo.

Uteuzi wa Maradona ni gumzo kwa kuwa mashabiki wengi wana hofu kama atafanikiwa, kwa kuwa amekuwa akifeli katika timu zote.

Dorados iko katika wakati mgumu, inataka kujikokoa kuteremka daraja lakini wadau wanaona Maradona amechukuliwa kwa mtazamo wa kibiashara zaidi.


Mjadala huo umekuwa mkubwa katika mji wa Sinaloa lakini unakwenda unasambaa nchini Mexico na wengi wanataka kuona kama Maradona atakuwa na mafanikio.

Pamoja na kuwa na kipaji, amekuwa akionekana si mtu makini hasa kutokana na kujihusisha na utumiaji wa madawa.



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic