September 12, 2018




Bosi wa benchi la Ufundi la Simba, Mbelgiji, Patrick Aussems ameutaka uongozi wa klabu hiyo, kumrudisha kundini beki wake kati, Mganda, Juuko Murshid baada kuvutiwa na uwezo wake.

Kocha huyo alimuona Juuko akiitumikia timu ya Taifa ya Uganda kwenye mchezo wa kutafuta tiketi ya kufuzu kwa Kombe la Mataifa Afrika, juzi.

Juuko ambaye bado ana mkataba wa mwaka mmoja na Simba,  lakini hajaonekana katika kikosi hicho tangu kuanza kwa msimu huu kutokana na kile kinachodaiwa ni kutokuwa na maelewano mazuri na uongozi wa klabu hiyo.

Habari zimeeleza kuwa, baada ya Aussems kumuona, Juuko katika mchezo huo akipambana na vilivyo na washambuliaji hatari kama Mbwana Samatta aliuambia uongozi umlete mchezaji huyo.

“Amedai kuwa kwa jinsi alivyomuona anaamini kabisa Juuko atatusaidia sana katika michuano ya kimataifa kwani ana sifa zote anazotakiwa kuwa na nazo beki wa kati,” kilisema chanzo hicho cha habari.

Alipoulizwa Aussems kuhusiana na beki hiyo alisema kuwa: “Ni kweli nilimuona ni beki mzuri na ningependa kuwa naye kikosini kwangu, hata hivyo, nimeshawasiliana na viongozi kwa hiyo wao ndiyo wanajua nini cha kufanya.”

SOURCE: CHAMPIONI

1 COMMENTS:

  1. Inawezekana kabisa kuna chuki za mtu binafsi pale Simba juu ya suala la Juko Murshidi. Haingii akilini uende ukamuamini Paul Bukaba umuweke Juko benchi? Sio kwamba Bukaba si mchezaji mzuri la hasha ila hata yeye mwenyewe Bukaba anajua yakuwa anakosa vitu kadhaa vya kujifunza kukosekana kwa Juuko pale Simba. Kazi ya viongozi ni kusimamia na kutatua matatizo ya wanaowaongoza na kushindwa kwa kiongozi au viongozi kutimiza majukumu hayo basi taasisi fulani lazima itakubikwa na utata. Suala la Juuko si la leo na kama simba wanamkomoa hivi kwakuwa anamkataba wao la sivyo Yanga walishambeba zamani sana kama ilivyokuwa kwa Amisi Tambwe na hata Yondani. Simba imekuwa na tabia ya kuwapoteza wachezaji wazuri wa kuweza kuisaidia timu kizembe.Kama Juuko ana matatizo nje ya taaluma yake ya kusakata soka kwanini viongozi wake wasikae nae chini na kuzungumza nae na ikiwezekana tumsikie yeye mwenyewe binafsi Juuko tatizo lipo wapi maana sidhani kama Juuko alishapata nafasi ya kujieleza mbele ya wapenzi na wanachama Simba kuhusiana na tuhuma dhidi yake tunachosikia ni kauli za viongozi tu. Licha ya mechi ya Taifa Stars dhidi ya Uganda nilibahatika kumuona Juko pale Uganda dhidi ya Egypt ni vitu visivyoingia akilini kuamini kuwa alikuwa akindesha shughuli zake za kucheza soka nchini Tanzania.Hata kama wakisema sijui Juuko anaringa basi anachokitu cha kuringia sio hivi hivi tu ni kazi ya uongozi kumuweka sawa au kumuacha aende wavunje nae mkataba akatafute riziki sehemu nyengine ili kulinda kipaji chake kuliko kumuekea kauzibe .

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic