KOCHA COASTAL UNION AZISHANGAA TIMU LIGI KUU, AMTAJA ALI KIBA
Kocha Mkuu wa timu ya Coastal Union, Juma Mgunda, ameibuka na kueleza hakuna timu yoyote inayoweza kushinda mechi zote za ligi popote pale.
Mgunda ametoa kauli mapema baada ya kumalizika kwa mazoezi ya timu hiyo jana kuelekea mechi zijazo za ligi kuu bara.
Kocha huyo ameeleza kuwa maandalizi yao yanaenda vema na akieleza katika mchezo wa mpira lazima kuwe na matokeo ya aina tatu na si kushinda pekee.
"Hakuna timu ambayo inashinda mechi zote, ni jambo la kushangaza kwa maana kama ipo basi hiyo itakuwa si ya mpira, maandalizi tunayoyafanya kwa sasa tunaamini tutapata matokeo kuelekea mechi zijazo" alisema.
AIdha, Mgunda amemtaja straika wake Ali Kiba kuwa anatarajiwa kuwa sehemu ya kikosi kitakachocheza mechi ijayo baada ya kuanza tizi na wenzake.








0 COMMENTS:
Post a Comment