EXCLUSIVE: SIMBA YAMALIZA TOFAUTI NA JUUKO, MAMBO SASA NI MOTOO
Na George Mganga
Kaimu Rais wa wa Simba, Salim Abadallah, 'Try Again' amesema klabu hiyo imemaliza tofauti zake na beki wake raia wa Uganda Juuko Murshid.
Kwa mujibu wa Azam TV, Kaimu huyo ameeleza kuwa kwa sasa Murushid yuko huru kuitumikia klabu hiyo, huku mchezaji mwenyewe akiomba ushirikiano kutoka kwa wanachama na mashabiki wa timu hiyo.
Murushid ambaye hajacheza mechi hata moja msimu huu, alikuwa kwao Uganda na juzi aliibukia katika timu ya taifa lake kuitumikia The Cranes dhidi ya Taifa Stars kuwania tiketi ya kufuzu kuelekea AFCON.
Beki huyo anaweza akawa sehemu ya kikosi cha Simba kitakachofanya mazoezi kesho kwenye Uwanja wa Boko Veterani kujiandaa na mchezo wa ligi dhidi ya Ndanda FC.
Simba itakuwa mgeni kucheza na Ndanda Jumamosi ya wiki hii mjini Mtwara kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona.
Duh kumenoga msimbazi afadhali umerudi baba mwenye nyumba.
ReplyDeleteSafi sana kikosi kimetimia
ReplyDeleteHongera sana kaimu rahisi kwa kulitatua suala la Juuko. Uwepo kwako Simba hakika ni fahari kwa wanasimba wote kwani jitihada zako katika utendaje wako wa kazi kuhakikisha clabu inasonga mbele ni kubwa mno watanzania tunatamani TFF wangekuwa na kiongozi anaelingana na wewe kiutendaji. .
ReplyDeleteNi kiongozi wa vitendo maneno machache
Delete