September 16, 2018


Kocha Mkuu wa Simba, Mbelgiji, Patrick Aussems, ameuambia uongozi wa timu hiyo kuwa, anataka kuendelea kukaa hotelini kwa kuwa amezoea na pia hajui kupika.

Aussems jana Jumamosi aliiongoza timu hiyo kucheza dhidi ya Ndanda katika mchezo wa Ligi Kuu Bara ukiwa ni wa tatu kwake na wa kwanza wa ugenini katika ligi ya msimu huu ambao ulienda suluhu ya kutokufungana.

Ikumbukwe, Mbelgiji huyo alifikia katika Hoteli ya Golden Tulip ya Masaki kabla ya kuhamishiwa katika Hoteli ya Sea Scape iliyopo Mbezi Beach mara baada ya kuanza kazi kwenye timu hiyo na japo hulipa chumba Sh 170,000 kwa siku.


Kwa mujibu wa gazeti la Championi Jumamosi, Aussems alisema hawezi kukubali kuishi kwenye nyumba za kupangiwa kwa kuwa maisha yake ya ukocha amekuwa akiishi hotelini.

“Kwa hapa ndiyo sehemu ambayo nitaendelea kuishi kwa muda wote, nilishawaambia viongozi na hilo wanalijua hivyo siwezi kwenda kuishi kwenye nyumba yoyote zaidi ya hapa.

“Unajua kwanza sijui kupika halafu maisha ya hotelini nimeyazoea tangu nimeanza kufanya kazi Afrika nimekuwa nikiishi hoteli sawa na hapa na uzuri huwa sichagui chakula ili mradi kiwe kitamu,” alisema Aussems.

4 COMMENTS:

  1. Naiyona safari ya kwao inamuita ukichanganya na matokeo ya jana

    ReplyDelete
  2. Sijawahi kuiona simba ya kiwango kibovu kama ya Jana. Shem on you Patrick Aussems

    ReplyDelete
  3. Nimeuona umuhimu was Masoud Juma kwa kweli

    ReplyDelete
  4. KUNA JAMBO MOJA LAZIMA TUFAHAMU, KOCHA ANANAFASI YAKE. PIA WACHEZAJI WANANAFASI ZAO. KWA GAME YA JANA WACHEZAJI NDIO WAMETUANGUSHA. WANAANZA GAME KAMA VILE HAITAJI USHINDI. MUDA UMEKWENDA ZIMEBAKI DAK 20,15 NDO WANAANZA KUKOMAA.SISI MASHABIKI HATUPENDEZWI NA HIYO TABIA YA WACHEZAJI KUCHUKULI GAME POA AU KUZARAU BAADHI YA TIMU. HII TABIA KUZARAU BAADHI YA TIMU IMETUGHARIMU KWA MIAKA MINGI NA HATIMAYE KUPOTEZA MATAJI.JITIHADA ZA WACHEZAJI KUITAFUTIA TIMU YAO USHINDI NI LAZI ZIONEKANE KUANZIA DAKI YA 1 HADI DAK 90 YA MCHEZO.IKITOKEA HATUPATI MATOKEO MAZURI BASI IWE NI KWA SABABU YA WAPINZANI WETU NAO KUPAMBANA/KUWA VIZURI.WACHEZAJI WA SIMBA LAZIMA WABADILIKE, WAJIFUNZE KWA TIMU KAMA MAN CITY, WACHEZAJI WANAJITUMA MUDA WOTE UWANJANI NA TIMU INAPATA MATOKEO.HILI LA WACHEZAJI WETU KAMA UONGOZI, BENCHI LA UFUNDI NA WACHEZAJI WENYEWE WASIPOLIONA KWA HARAKA NA KUBADILIKA ITATUSABABISHA TURUDI KULE TULIPOKUWA MIAKA MITATU ILIYOPITA.TIMU KAMA IKASHINDWA KATIKA MAZINGIRA KUPAMBANA HUTUWEZI KUHAMAKI. JANA HATA SHOT ON TARGET TAABU.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic