September 4, 2018







Ile kampuni ya Star Media (T) Ltd kupitia king’amuzi chake cha StarTimes, imetangaza kurejea kwa Ligi Kuu ya Ujerumani maarufu kama Bundesliga ambapo kwa msimu wa 2018/19, chaneli zao zote za michezo zitaonyesha mechi zake kwa matangazo ya Kiswahili.

Akizungumza ujio huo mpya wa Bundesliga, meneja masoko wa kampuni hiyo, David Malisa, alisema: “Ikumbukwe kwamba StarTimes pekee ndio tunaonyesha Ligi ya Bundesliga na sasa burudani inaongezeka maradufu kwa sababu mechi zitatangazwa kwa lugha yetu ya nyumbani yaani Kiswahili.

“Pia tutatumia wachambuzi makini kabisa wenye weledi katika soka la Ulaya, bila ya kusahau mechi zote zitakuwa zikipatikana kwa kiwango cha HD kwenye chaneli zetu za michezo.”


Mbali na Bundesliga, StarTimes pia ni warushaji wa Ligi Kuu ya Ufaransa maarufu kama Ligue 1 ambapo Malisa aliongeza kwa kusema:

“Mechi zote za Bundesliga na zile za Ligue 1 zinapatikana kuanzia kifurushi cha MAMBO kwa Sh 13,000 kwa watumiaji wa antena.

“Kwa watumiaji wa Dish watashuhudia chaneli hizo zote kupitia kifurushi cha SMART, Sh 19,000 ambapo zinapatikana chaneli zetu za michezo yaani World Football, Sports Premium, Sport Focus ambazo zote zinapatikana kwa kiwango cha HD, hivyo wateja wetu wana uhakika wa kufurahia picha safi zaidi wanapokuwa wakitazama kandanda la Bundesliga na Ligue 1.”

Kwa upande wake Meneja Maudhui wa StarTimes, Zamaradi Nzowa, aliwatambulisha mastaa kadhaa ambao watafanya nao kazi katika kuhakikisha taarifa zinafika kwa wakati kwa wateja ambao muda mwingi wanakuwa katika mitandao ya kijamii. Baadhi ya mastaa hao ni Madee, Dogo Janja na Mkali wenu.


Caption
1. Meneja Masoko wa StarTimes, David Malisa akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani). Pembeni yake ni Meneja Maudhui wa StarTimes, Zamaradi Nzowa.
2. Madee ambaye ni mmoja wa mastaa wanaotumiwa na StarTimes kuitangaza Bundesliga, akizungumza jambo.
3. Dogo Janja Madee ambaye ni mmoja wa mastaa wanaotumiwa na StarTimes kuitangaza Bundesliga, akizungumza jambo.
4. Baadhi ya Wafanyakazi wa StarTimes wakiwa katika picha ya pamoja na mabalozi wao wanaowatumia kwa ajili ya kuitangaza Bundesliga.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic