September 5, 2018


Kipa aliyeng'ara kwenye mashindano ya SportPesa Super Cup nchini Kenya, Manyika Peter, imeelezwa kuwa ameamua kuvunja rasmi mkataba wake kutokana na kutotimiziwa stahiki muhimu.

Kipa huyo ambaye alisajiliwa na Singida United akiwa kama mchezaji huru baada ya kumaliza mkataba na Simba, amesema kuna baadhi ya stahiki ikiwemo fedha zake za usajili kushindwa kulipwa.

Kitendo hicho kimefanya Manyika aamue kuvunja mkataba huo na sasa amebakia huru hivyo klabu yoyote inaruhusiwa kufanya naye mazungumzo.

Aidha, hapo awali baada ya taarifa za kutolipwa fedha za mchezaji huyo, uongozi Singida uliwahi kusema wanaendelea na mazungumzo wa kuhakikisha kila kitu kinakaa sawa.

Manyika aliingarisha Singida kwenye SportPesa Super CUP nchini Kenya iliyofanyika miezi kadhaa iliyopita na kuiwezesha kumaliza ikiwa mshindi wa tatu.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic