September 5, 2018


Uongozi wa klabu ya Yanga kupitia Kaimu Katibu Mkuu wake, Omary Kaaya, umemkingia kifua Kocha wake mkuu, Mwinyi Zahera, kutokana na kuendelea kukaa jukwaani wakati wa mechi.

Kaaya ameibuka na kueleza kuwa suala la Zahera kutokaa kwenye benchi la ufundi halina maana kuwa timu haiwezi kupata matokeo na badala yake ni wachezaji wenyewe wanawajabika wakiwa Uwanjani.

Kaimu huyo ameongea kwa msisitizo akisema hata kama Zahera angekuwa anakaa kwenye benchi la ufundi hakungekuwa na utofauti wowote ule na akiwa jukwaani kwa maana tayari anakuwa ameshawaandaa wachezaji wake.

Aisha, Kaaya amesema Zahera si mchezaji kwakuwa hata kama akiwa kwenye benchi hawezi kuingia uwanjani na kucheza kwasababu hana mamlaka hayo bali ni kwa wachezaji pekee.

Vilevile Kaaya amefunguka na kueleza kuwa watu pekee wanaopaswa kuuliza kama Zahera amepata kibali cha kazi ni idara ya uhamiaji na si wengine.

Wakati Kaaya akisema hayo, Kocha Zahera alionekana mara ya kwanza akiwa amekaa kwenye bechi la ufundi wakati Yanga ikikipiga na Rayon Sports kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika huko Kigali, Rwanda.

1 COMMENTS:

  1. Wakati mwingine huyu kiongozi mbabaishaji wa Yanga inabidi akae kimya bila kusema utumbo usiokuwa na maana.Kwanini timu zinamlipia kocha kama hana faida ya kukaa benchi?Kwa mantiki yake kocha hana maana kwani wanaocheza ni wachezaji.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic