MKONGO YANGA AIPIGA DONGO HILI SIMBA
Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera ameeleza dhamira yake ya kuhakikisha anafanya vizuri msimu huu kwa kuhakikisha anashinda kila mechi atakayocheza, huku akisema haifuatilii Simba.
Zahera kwa sasa yupo na timu ya taifa ya DRC Congo ambapo ni kocha msaidizi iliyopo nchini Liberia kuvaana na timu ya taifa ya nchini humo katika mechi za Kuwania kushiriki Afcon keshokutwa Jumapili usiku.
Yanga kwa sasa ipo nafasi ya 10 ya msimamo wa ligi kwa kuwa na pointi tatu ikiwa na michezo miwili mkononi, baada ya kucheza mechi moja tu.
Kwa mujibu wa Championi Ijumaa, Zahera kutoka Liberia, amesema kuwa, anachohitaji ni kuona timu yake inafanya vizuri kwenye ligi na ikiwezekana kushinda kila mchezo ili kuweza kujiweka katika nafasi nzuri ya msimamo wa ligi.
“Ligi ni ngumu na ina ushindani wa hali ya juu, tunahitaji kufanya vizuri katika mechi tutakazocheza, nitakiandaa kikosi changu kuona tunafanikiwa kushinda kila mechi ili tuweze kuwa juu, kuhusu Simba siwezi kuizungumzia kwa kuwa siifuatilii hata kidogo, nazifuatilia timu nyingine.
“Nimeandaa programu ambazo zinaendelezwa kipindi hiki chini ya kocha msaidizi, naamini kila kitu kitakwenda sawa,” alisema Zahera ambaye familia yake inaishi Ufaransa.








Huyu kocha ana msongo wa mawazo unaosababishwa na kulipwa mshahara kiduchu na yanga,anazidiwa hadi na msaidizi wake huku mshahara wa mbelgiji mmojawa simba ukichanganywa na ule wa mholanzi wa azam unatosha kumlipa yeye mwaka mzima.
ReplyDeleteUsikariri kwenye michezo unaweza kulipwa pesa nyingi lkn ukawa bure tu huna lolote mbona kichuya mshahara wake ulikuwa mdogo lkn alikuwa anapiga kazi ambayo uwezi kulinganisha na Niyonzima alichofanya?
DeleteUnaweza kulipwa pesa nying ukawa na mawazo unachokifanya na pesa ulnayopewa haviendani tatizo ushabiki uchwara mlionao baadhi ya watu hamfikirii kwa kina.
Ligi bado tutajua hiyo kocha wa kishansha mwenye nusu mshahara wa masudi Juma anafanya kazi kweli.Na pia tutajua kuwa kuwa na kocha anayekaa jukwaani Siku timu take inacheza ana ufanisi wowote
Deletewe mbulula kweli.....hao makocha sioni tofauti ya viwango vyao ktk ufundishaji lakini mmoja analipwa kidogo mwingine analipwa zaidi,sasa hapo wenye akili na wajanja nani kati ya yanga na simba.we inaonekana hata hesabu ndogo za primary huziwezi.....ndo nyinyi mmnaenda kariakoo mmnauziwa suruali kwa elfu 50 ambazo wengine wanazinunua kwa elfu 15 lakini mnajiona wajanja eti kwakuwa mna hela za kulipa zaidi.
Deletewanaofatilia simba na yanga ni nyinyi waandishi ili muuze magazeti
ReplyDeleteMbona kocha wa Simba haizungumzii kabisa Yanga.anatakiwa kujali ya Yanga na sio Simba
ReplyDelete