September 2, 2018


Nyota na nahodha wa zamani ya Simba, Mussa Hassan Mgosi, ameshangazwa na kikosi cha timu hiyo kutokana na mwenendo ilioanza nao, imeelezwa.

Mgosi ambaye aliwahi kung'aa na kutamba na timu hiyo wakati akiichezea, amesema kwa namna walivyoanza ligi inampa mashaka kutokana na usajili ilioufanya.

Mgosi ameeleza kuwa kikosi cha Simba kilichosajiliwa kimewapa imani kuwa wapenzi, mashabiki na wanachama wake kufanya vizuri zaidi kwa namna uongozi ulivyosajili kikosi kipana.

Licha ya kikosi kipana kusajiliwa, Mgosi ameeleza kuwa anapatwa na mashaka kwa namna ambavyo Simba imeanza kwa mechi mbili dhidi ya Tanzania Prisons na Mbeya City kwa ushindi kiduchu.

Mchezajji huyo wa zamani ameshauri ifikie wakati wachezaji watambue thamani ya Simba na kile walichokitarajia mashabiki waweze kukionesha na kuonesha upana wa kikosi kilichopo hivi sasa.

4 COMMENTS:

  1. Naona wadau wasiwe na papara na kuanza kuwakoroga wachezaji. Sijui kama Simba ingelipoteza katika mechi hizi mbili wadau wangeripuka kiasi gani? Kweli Simba kwa sasa kuna mazingira mazuri ya timu ya ushindi kulinganisha na timu nyengine lakini kila timu lazima ifahamike inaingia uwanjani kwa ajili ya kushinda,iwe lipuli,ndanda au biashara wote wanaingia uwanjani kupambana kushinda mechi na dio malengo katika mikakati ya kuinua kiwango cha soka nchini kuwa kila timu ipambane haswa haihalisi wanacheza na nani. Ushindani wanaoupata Simba ni wa afya sana kuelekea mechi za kimataifa kwa hivyo wadau tusiwe walaini sana wa kuzichukulia timu nyengine kuwa za kupigwa tu tena kwa mabao mengi na Simba.

    ReplyDelete
  2. Amesahau yeye alicheza msimu mzima akizidiwa magoli na dida na tulimvumilia,au anafikiri tumesahau

    ReplyDelete
    Replies
    1. 😂😂😂😂 . Anataka kutuletea pressure kwa wachezaji wetu.. pumzika kwa amani Mgosi, Simba imecheza mara 2 na in points 6. Hivi wewe si hujui kuwa mwalimu akiwa mpya timu inachelewa ku peak? Be like a professional footballer bro.

      Delete
  3. Enter your comment...timu zingine nazo zinajiandaa tushukuru kwa ushindi kwaani barcelona kwa hela anayotumia mbona anafungwaga na levante,espanyol huu ni mpira mwisho wa siku ni dakik 90

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic