September 4, 2018




Mshambuliaji Saimon Msuva, ameweka rekodi baada ya kutua nchini moja kwa moja na kwenda uwanjani kuanza mazoezi na kikosi cha Taifa Stars.

Msuva amejiunga na kikosi cha Taifa Stars kilichokuwa mazoezini kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam baada ya kutua akitokea Morocco anapokipiga katika kikosi cha Difaa Al Jadida.

Mshambuliaji huyo wa zamani wa Yanga aliwasili Uwanja wa Taifa akiwa na begi lake, alipitiliza vyumbani na kuanza maandalizi kabla ya kuungana na wenzake chini ya Kocha Emmanuel Amunike.

Pamoja na Msuva, nahodha wa Taifa Stars, Mbwana Samatta ameungana na wenzake katika mazoezi ya timu hiyo.

Samatta anayechezea KRC Genk ameanza mazoezi na wenzake akiungana pia na Thomas Ulimwengu ambaye anacheza Al Hilal pamoja na wengine wanaocheza nje ya nchi.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic