September 12, 2018


Aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage, ameshangazwa na maamuzi ya klabu hiyo kushindwa kutoa elimu kinagaubaga juu ya elimu ya katiba mpya.

Hatua hiyo imekuja mara baada ya baadhi ya wanachaa kuanza kutupia lawama juu ya katiba hiyo wakati wa zoezi la kuchukua fomu za kugombea nafasi mbalimbali kuelekea uchaguzi mkuu.

Rage ameeleza kuwa yawezekana Simba wamejichanganya kwa kufanya haraka kutisha uchaguzi kabla ya kuwapa elimu vizuri wanachama ili waweze kuielewa vema namna katiba ilivyo.

Kiongozi huyo mstaafu anaamini suala hilo limesababisha baadhi ya wanachama kushindwa kujitokeza kuchukua fomu sanjari na ada ambayo ilikuwa imewekwa.

Kiasi cha ada ambayo ni shilingi za kitanzania laki tano kimemfanya Rage aaamini wanachama wengi kushindwa kufika makao makuu ya klabu kuchukua fomu sababu ni kubwa.

Mwanachama huyo ameeleza ifikie hatua klabu ilipaswa kuangalia na namna hali ya Mtanzania ilivyo ili kila mwenye sifa aweze kuimudu lakini kwa sasa ni sawa na kutwanga maji kwenye kinu kwa maana muda tayari umeshapita.

2 COMMENTS:

  1. tatizo hawa wanachama wamezoea kufata mkumbo wanashindwa kutumia haki yao ya kikatiba kuhoji kama jambo hawakubaliani nalo, kabla ya katiba kubadirishwa ilipaswa kusambazwa mapema na wanachama wakajadili kipengele baada ya kipengele kwa mfano Simba ilianzishwa kama klanu ya michezo ndio maana kuna kipindi Simba ilikuwa na timu mpaka ya ngumi lakini katiba mpya imegeuza simba ni klabu ya mpira wa miguu na itafata na ktii kila kitu kinachoamriwa na tff na fifa kwa maana nyingine wamejipoka madaraka yao na kuyakabidhi kwa mamlaka nyingine na uhakika hata haji manara hajaisoma hii katiba kwani kuna kipengele kinasema sifa ya mwanachama ni kuwa mwaminifu kipengele hiki baadhi ya wanachama wanaweza kukitumia kumfuta uwanachama haji manara kwani wote tunajua Haji Manara ni sababu gani ilimtoa ukatibu uenezi wa CCM mkoa wa Dar es salaamj

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic