SIMBA YAGEUZA KIBAO KANDA YA ZIWA, YAITANDIKA MWADUI 3-1, BOCCO NA KAGERE KAMA KAWA
Na George Mganga
Safari ya Kanda ya Ziwa imemalizika na furaha leo kunako dimba la CCM Kambarage Shinyanga kwa wekundu wa Msimbazi, Simba kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Mwadui FC.
Mabao pekee ya Simba yamewekwa kimiani na Nahodha John Bocco aliyringia kambani mara mbili mnamo dakika za 41 kwa njia ya penati iliyotaka na kufanyiwa madhambi eneo la hatari kisha kufunga tena dakika ya 45.
Bao la tatu la Simba liliwekwa kimiani na straika mwenye balaa la aina yake Meddie Kagere katika dakika ya 51 ya kipindi cha pili na kumfanya afikishe jumla ya mabao manne msimu huu tangu uanze.
Wakati huo bao pekee la mwadui FC lilipachiwa kiminia na Charles Ilanfya katika dakka dakika ya 82 kipindi cha pili ikiwa ni mapema baada ya Nahodha wa Simba, John Bocco kupewa kadi nyekundu iliyotokana na kumpiga ngumi mchezaji wa Mwadui FC.
Baada ya mechi hiyo, Simba wataanza rasmi maandalizi kujiandaa na mchezo ujao dhidi ya watani zao wa jadi Yanga utakaopigwa Septemba 30 2018.
0 COMMENTS:
Post a Comment