NIZAR KHALFAN ACHUKUA MAJUKU YA MFAUME NA CHALLE
Baada ya makocha wasaidizi wa klabu ya Singida United Athuman Mfaume na Jumanne Chale kuachia ngazi kwa sababu za madai ya mshahara, imeelezwa kuwa aliyekuwa Nahodha wa timu hiyo, Nizar Khalfan amechukua mikoba yao.
Hatua hiyo imekuja kutokana na benchi hilo la ufundi kukosa Mwalimu Msaidizi na kubakiwa na Hemed Morocco kama Kocha Mkuu pekee.
Baada ya Chale na Mfaume kuachia ngazi, uongozi wa Singida ulikaa na kuzungumza na Khalfan kisha kumpa nafasi hiyo ya kumsaidia Morocco majukumu ya kazi kwa ajili ya kuinoa Singida.
Nizar atakuwa sehemu ya benchi la ufundi leo wakati timu yake itakapokabiliana na Yanga majira ya saa 1 za usiku Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Sana mimi naitakia kila raheli timu ya singida ushindi upo tu
ReplyDelete