September 20, 2018


Uongozi wa klabu ya Simba kupitia kwa Mwenyekiti wa Uchaguzi, Boniphace Lihamwike, umesema kuwa mpaka sasa hawajapokea barua yoyote kutoka TFF inayowataka kusimamisha mchakato wa uchaguzi wao.

Lihamwike amesema kufikia mpaka sasa wanaendelea na zoezi la usaili wa wanachama wote waliorejesha fomu zao kuelekea kampeni tayari kwa uchaguzi ambao utafanyika Novemba 3 2018.

Mwenyekiti huyo amesema ukiachana na kupokea barua hiyo, ameeleza kuwa TFF imewaomba kutumiwa majina ya wagombea wote pamoja na nyadhifa zao ili kujua namna mchakato huo unavyoenda.

Kiongozi huyo amesema TFF wanahitaji majina hayo wakiwa kama nguzo ya soka la Tanzania ili kujua pia hatua ambayo kama klabu imefikia.

Lihamwike ameeleza kuwa zoezi la usaili linazidi kushika kasi na mchakato wa uchaguzi huo unazisdi kupamba moto kabla ya tarehe ya uchaguzi kufika.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic