September 12, 2018


Wakati Yanga wakiwa katika sintofahamu ya kufanya uchaguzi mkuu, Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limesema lipo njia panda juu ya kinachoendelea ndani ya klabu hiyo mpaka sasa.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya Shirikishi hilo, Wakili Revocatus Kuuli, amesema wao kama TFF bado wapo njia panda kwa maana walisema watamrejesha Yusuf Manji kuwa Mwenyekiti wao.

Kuuli ameeleza wao kama TFF walitoa siku 75 kwa Yanga na Simba kuanza michakato ya kujiandaa na chaguzi zao lakini baadaye Yanga wakasema wao bado wanamtambua Manji kuwa ndiye Mwenyekiti.

Mwenyekiti huyo amefunguka kuwa TFF inashindwa ifanye maamuzi yapi kutokana na suala hilo kuchanganya mambo baada ya Manji ambaye baadaye alitangaza kuachia ngazi hiyo kuja kuelezwa tena anarejeshwa.

Mpaka sasa Manji licha ya kuhudhuria mechi ya kimtaifa ya Kombe la Shirikisho kati ya Yanga dhidi ya USM Alger Uwanja wa Taifa Dar es Salaam, bado hajatoa tamko la kurejea kwake kwenye nafasi hiyo ya Uenyekiti.

3 COMMENTS:

  1. WANA JANGWANI HEBU JARIBUNI KUUKUBALI UKWELI NA UHALISIA WA MAMBO,KWANINI MNAMLAZIMISHA MTU KUKALIA KITI AMBACHO HAKITAKI??MANJI ALIKWENDA TAIFA KAMA MSHABIKI WA KAWAIDA WA YANGA KUANGALIA MPIRA,LAKINI CHA AJABU WANA JANGWANI WAKAZUSHA ETI AMERUDI,LEO MNATULETEA HABARI ZA KIPUUZI KAMA HIZI,BLOGA UNAJIHARIBIA CREDIBILITY MY BROTHER TRY TO BE ACCURACY,KAMA TUKIJARIBU KUFANYA UTAFITI(RESEARCH)KWA HII BLOG YOU WILL FIND ALOTS OFF LIES AND NONCONFIRMED INFORMATIONS,KAA UKIJUA HII BLOG INASOMWA AROUND THE GLOBE SASA UKIWA UNAFANYA KAZI NA AGENTS WASIOKUA WA UHAKIKA NA VYANZO VYA HABARI SUBIRI KUANGUKIA PUA MUDA SI MREFU,PIA PUNGUZA KUDHIHIRISHA RANGI YAKO HALISI HII ITAKUFANYA KUA NA VIEWRES WENGI SANA,SIO LAZIMA KUCHUKUA USHAURI WETU ILA KAMA UTAUONA UMUHIMU WAKE UNAWEZA UKAUFANYIA KAZI.AHSANTE

    ReplyDelete
  2. Ni juu ya TFF kumuandikia Manji easmi aeleze msimamo wake kuliko kukubali kuyumbishwa.

    ReplyDelete
  3. HII TFF NAO SHIDA. MTU AMEJIUZULU KWA BARUA YA WAZI, MWAKA UMEPITA, KAIMU MWENYEKITI AKATEULIWA TFF KUWA MWENYEKITI WA KAMATI MOJAWAPO TFF NAYE KAJIUZULU UONGOZI YANGA, LEO MNAAMBIWA MANJI AMERUDI KUWA MWENYEKITI KWELI TFF MNASHINDWA KUHOJI UTHIBITISHO KIMAANDISHI KUTOKA YANGA? BADALA YAKE MNASEMA MPO NJIAPANDA? ENDESHENI MAMBO KIHAKI NA KIOFISI. HIVI KUIACHA YANGA BILA MWENYEKITI MUDA WOTE HUU KUNA MASLAHI GANI KWA KLABU NA TAIFA?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic