September 5, 2018


Zikiwa zimesalia siku nne pekee kuelekea pambano la Taifa Stars dhidi ya Uganda, Kocha Mkuu wa Stars, Emmanuel Amunike, amekongwa nyoyo na ujio wa wachezaji wa kimataifa.

Amunike amesema amefarijika zaidi kuwaona kutokana na baadhi alikuwa akiwasikia tu na hakuwahi kukutana nao ikiwemo Mbwana Samatta anayekipiga huko KRC Genk, Ubelgiji.

Kocha huyo ana imani ujio wa wachezaji hao utaweza kuwapa changamoto Uganda kwenye mchezo wa kuelekea kufuzu AFCON utakaopigwa Uganda.

Stars itakuwa mgeni kwenye Uwanja wa Nambole huko Kampala Septemba 8 2018 tayari kuanza kusaka tiketi hiyo.

Baadhi ya wachezaji waliowasili ambao wanakipiga nje ni pamoja na Rashid Mandawa, Thomas Ulimwengu, Simon Msuva, Abdi Banda, Shaban Idd, Farid Mussa, Hassan Kessy na Himid Mao.

Wakati kikosi cha Stars kimezidi kujifua na mazoezi ya kufa mtu kwenye Uwanja wa Boko Veterani uliopo pembezoni kidogo mwa jiji la Dar es Salaam tayari kuelekea mechi hiyo.

2 COMMENTS:

  1. Taswira fupi kuelekea mechi kati ya Uganda na Taifa Stars. Mechi za mwanzo katika kundi lao kundi lao Mganda kampiga Cape Verde kwao goli moja mtungi. Tanzania akatoka sare na letheso Daresalam mbele ya halaiki yake 1-1.

    ReplyDelete
    Replies
    1. wewe bando umeganda na ya miezi kadhaa iliyopita?.....inawezekana tanzania tukafungwa lakini hiyo taswira yako siyo kigezo kwakuwa ya miezi ile yanaweza yasiwe ya mwezi huu......siku haziganda ndugu.

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic