September 11, 2018


Imeripotiwa kuwa beki wa timu ya Taifa ya Ufaransa na Barcelona, Samwel Umtiti ametoa siri kuwa wachezaji wote wa Ufaransa juu ya kuwa na woga kwa mechi dhidi Argentina hatua robo fainali ya Kombe la Dunia 2018 huko Urusi.

Taarifa imeeleza wachezaji wa Ufaransa walikuwa wanajiuliza nani ataweza kumkaba Messi kutokana na umaridadi wake wa kucheza na mpira.

Umtiti ameibuka na kufichua siri kwa kumtaja Ng’olo Kante kuwa aliomba jukumu la kukabiliana na Messi ili apunguze makali yake.

Beki huyo wa Barcelona amefichua siri hiyo ikiwa ni miezi mitatu sasa imeshapita tangu kumalizika kwa michuano hiyo ambapo Ufaransa walifanikiwa kuwa mabingwa.

Kitendo cha Kante kumkaba Messi kilisababisha Kante kuimbiwa nyimbo za furaha baada ya kutwaa taji hilo kubwa duniani.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic