September 12, 2018


Uongozi wa klabu ya Yanga kupitia kwa Katibu wa Uchaguzi, Bakili Makele, umesema hauwezi kufanya kazi zake kwa kuziiga timu nyingine kuhusiana na mchakato wao wa uchaguzi.

Kwa mujibu wa EFM, Makele amesema suala la wao kufanya uchaguzi litafanyika wakati ukifika kwa maana badi wanaendelea na taratibu hizo na mambo yakishakuwa sawa kila kitu wataweka hadharani,

Katibu huyo ameeleza kuwa si kwamba kwa sababu tayari Simba wameshaanza mchakato huo na wao wawaige, bali wanafanya kwa taratibu maalum ambazo wao wamejipangia.

Tangu kutolewa siku 75 na Shirikisho la Soka Tanzania kwa vilabu vya Simba na Yanga, mpaka sasa hakuna dalili zozote zinazoonesha kwa klabu hiyo bingwa kihistoria wa Ligi Kuu Bara kuanza harakati za uchaguzi.

TFF iliwapa siku 75 Simba na Yanga kuanza mchakato huo ili uchaguzi uweze kufanyika tayari kuwapata viongozi wengine ambao watakuwa watawala kwa muda ambao katiba zao zinasema. 

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic