September 8, 2018


Wakati tukisuburia pambano la kuwania kufuzu AFCON kati ya Uganda The Cranes dhidi ya Taifa Stars, unaambiwa changamoto kubwa inayowakabili wachezaji wengi wa kiganda ni lugha ya Kiswahili.

Taarifa ambazo imezipata Saleh Jembe kutoka Kampala, inasema wachezaji na wakazi wengi wa taifa hilo wanapatwa na ugumu wa kuzungumza Kiswahili.

Wachezaji wengi wanaokipiga katika timu hiyo ya The Cranes ukiachilia wale wanaosakata kambumbu katika vilabu vya Tanzania wamekuwa wakizungumza Kiingereza zaidi.

Mbali na wanaocheza kambumbu hapa nchini akiwemo Emmmanuel Okwi na Juuko Murushid ambao wanajitahidi, wakazi pia wa nchi hiyo asilimia kubwa ni wazungumza Kiingereza.

Taarifa zinasema kuwa ukiachana na Okwi pamoja na Juuko, wachezaji wa zamani pia waliowahi kucheza Tanzania ndiyo wanaweza kuzungumza Kiswahili kiasi kama George Owino.

The Cranes na Stars zinashuka dimbani majira ya saa 10 jioni jioni kukipiga kwenye Uwanja wa Mandela jijini Kampala.


2 COMMENTS:

  1. Hii inahusiana vipi nä mechi?Jamani blogu kila siku inakuja na utumbo unaozidi uliopita.

    ReplyDelete
  2. Hii blog imetuchoka kama huna taarifa basi kaa kimya tunatumia Mb zetu zen unaandika utumbo no fact

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic