October 2, 2018


Meneja wa Manchester City Pep Guardiola ameka nushataarifa kwamba anataka kumnunua mshambuliaji wa Paris St-Germain Kylian Mbappe, 19. (Independent)

Bodi ya Barcelona imagawanyika kuhusu ikiwa itamwendea kiungo wa kati wa Manchester United Paul Pogba, 25 mwezi Januari lakini mabingwa hao wa Uhispania wanaamini wana uwezo wa kifedha wa kutosha kuweza kumsaini Mfaransa huyo mshindi wa Kombe la Dunia. (ESPN)

Real Madrid wamejiunga katika kundi la klabu zinazomzea mate mchezaji wa kimataifa wa Wales Aaron Ramsey, 27, ambaye atondoka Arsenal mwezi January. (Teamtalk)

Arsenal ni kati ya vilabu vinavyommezea mate mchezaji wa Lille, Nicolas Pepe, 23.


Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ivory Coast mwenye thamani ya pauni milioni 30 amepokelewa vizuri chini Ufaransa kwa mchezo wake mzuri msimu huu baada ya kufunga mabao matano katika mechi nane.

Chelsea wako katika nafasi nzuri ya kumsaini mchezaji mwenye miaka 15 wa Volendam Mholanzi Sam Lautenschutz. (The Sun)


Wolves wanamwinda mlinzi wa Aberdeen raia wa Scotland Scott McKenna. Ofa za Celtic na Aston Villa zimekataliwa kwa mchezaji huyo mwemye miaka 21. (Scottish Sun)

Kiungo wa kati wa zamani wa Manchester United Lee Sharpe anaamini meneja wa klabu Jose Mourinho anastahilia kufutwa ikiwa matokeo yao mabaya yataendelea kwa mechi zao mbili wiki hii. (Talksport)


Meneja wa zamani wa Real Madrid Zinedine Zidane anariptiwa kumpigia simu Mourinho kumhakikishia kuwa hakuna mipango ya kuchukua mahala pake. (Mirror)

Mourinho anaaminiwa kutengwa huko Old Trafford baada ya kutofautiana na nahodha wa timu Antonio Valencia. (Mail)


Mshambuliaji wa United Alexis Sanchez, 29, alibaki akiteta baada kuachwa nje ya mechi na Mourinho kwa mechi wa wikendi na West Ham. (Mirror)

Kutoka BBC

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic