BILLNASS AFUNGUKA BIFU LAKE NA DOGO JANJA
Baada ya kutupiana maneno ya kashfa mitandaoni na msanii mwenzake, Abdulaziz Chende ‘Dogo Janja’ ambayo yalizua gumzo kwamba wawili hao wana bifu kali, mwana-muziki William Lyimo ‘Billnass’ ameibuka na kufunguka.
Awali Dogo Janja aliandika maneno kwenye ukurasa wa Billnass ambayo yalisomeka hivi; ‘Wewe ndiyo maana uliachwa na dada una mdomo sana, hamna mwanamke anaweza kukaa na mwanaume anachamba kuliko mwanamke’, baada ya muda Billnass naye alijibu kwa kuandika; ‘bora kuachwa kuliko kuolewa na mwanamke ili ucheze na mwanaye yeye akienda outings’.
Showbiz lilimtafuta Billnass ili azungumzie ishu hiyo ambapo alisema hana bifu na Dogo Janja bali maneno hayo yalikuwa ni utani tu.
“Sina bifu na Dogo Janja, hayo maneno tuliyokuwa tunaandikiana yalikuwa ni utani tu, sisi tumeshazoea kutaniana kwa hiyo nawaomba mashabiki zangu wasichukulie kwamba tuna tofauti,,” alisema Billnass.
SEMA BILINENGA MZEE WA KUPIMA OIL..........UNA MANENO YA KUUDHI ..NDO NINI KUMWAMBIA MWENZIO.....AMEOLEWA ILI ACHEZE NA MTOTO........
ReplyDelete