BREAKING NEWS: MZEE YUSUF AFIWA NA MAMA YAKE, AZIKWA UNGUJA
Aliyekuwa mwanamuziki wa nyimbo za taarab nchini, Mzee Yusuph, amefiwa na mama yake mzazi, Mwajuma Mzee.
Taarifa kutoka kwa dada wa Mzee Yusuph aitwaye Hadija Yusuph imesema mama yao alifariki nyumbani kwake Michezani kisiwani Unguja, Zanzibar, jana jioni na kuzikwa leo saa nne asubuhi katika makaburi ya Mwanakwereke kisiwani humo.
0 COMMENTS:
Post a Comment