October 14, 2018


Timu ya Manchester United ina mpango wa kumuongezea mkataba wa David de Gea kwa lazima miezi sita mapema kwa kutumia kifungu kilicho kwenye mkataba wake wa sasa, kama goli kipa wa Spain hataafikiana mkataba mpya na klabu hiyo kabla ya mwezi Januari. (Sun)

Mshambuliaji wa Wales,Gareth Bale, 29 amejipanga kukabiliana na juhudi zozote zile za Real Madrid kutaka kumlazimisha ahamie Manchester United majira mwishoni mwa msimu huu.

Juventus inaweza kumtaka kiungo wa Arsenal na Wales Aaron Ramsey, 27, kama watashindwa kumpata kiungo wa Ufaransa anayechezea Paris St-Germain Adrien Rabiot, 23. (Express)

Kuna taarifa kuwa Manchester City walitaka kumlipa mara tatu zaidi ya kiwango anacholipwa kwa sasa mchezaji nyota wa Barcelona na Argentina Lionel Messi, 31, kama angekubali kusaini mkataba nao. (Mundo Deportivo kupitia Sun)


Messi anaweza kuondoka Barcelona mwaka 2020 lakini mkataba wake unaeleza kuwa kama ataondoka basi hataruhusiwa kujiunga na timu nyingine "kubwa". (Mundo Deportivo)

Bingwa wa soka kutoka Argentina Diego Maradona amedai kuwa Messi sio kiongozi kwa sababu huwa anaenda maliwatoni mara 20 kabla ya mechi kuanza.(La Ultima Palabra kupitia Standard)


Antonio Valencia anakaribia kuihama Manchester United bila malipo yoyote kutokana na kifungu kilichopo kwenye mkataba wake. Mchezaji huyo Ecuador anaweza kusaini mkataba mpya katika klabu nyingine kuanzia mwanzo wa mwezi machi. (Sun)

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic