DE GEA, KANE, MOURINHO, MANCHESTER, MADRID: TETESI KUBWA NA BORA ZA SOKA ULAYA LEO
Real Madrid inapania kumsajili mshambulizi wa Tottenham na England Harry Kane, lakini huenda ikashindwa kumnunua mchezaji huyo wa miaka 25 ambaye gharama ya kumsajili ni Euro milioni 200 (El Confidencial - in Spanish)
Manchester United inakabiliwa na kibarua kigumu kumshawishi kipa wa Uhispania David de Gea, 27, kusalia Old Trafford baada ya kandarasi yake ya sasa kumalizika.(Telegraph)
Vilabu kadhaa zinazo shiriki ligi ya Premier vinammezea mate winga wa Borussia Dortmund Jadon Sancho, lakini huenda dau la mchezaji huyo wa miaka 18 likapanda zaidi ya Euro 100 baada ya kuitwa na England wiki hii. (Sun)
Meneja wa Manchester United Jose Mourinho anataka kumsajili mlinzi wa Inter Milan na Slovakia Milan Skriniar pamoja na beki wa kati wa AC Milan Alessio Romagnoli, mwezi Januari. (ESPN)
Maafisa wa Manchester United walikua nchini Ureno kuwafuatilia wachezaji kadhaa wa Benfica siku ya Jumapili. (Manchester Evening News)
Mshambulizi wa Everton Cenk Tosun anajiandaa kurejea Besiktas, ambao huenda wakamchukua mchezaji huyo wa kimataifa wa Uturuki wa miaka 27 kwa mkopo mwezi Januari. (MyNet, via Talksport)
Mshambulizi wa Genoa Krzysztof Piatek anafahamu fika kuwa Barcelona inataka kumsajili lakini kuna fununu kwamba Manchester City, Tottenham Hotspur na Liverpool pia zinafuatilia jinsi sogora huyo wa mika 23 raia wa Poland anavyosakata kabumbu. (Diario Sport, via Talksport)
Kiungo wa kati wa Manchester United Ander Herrera, 29, huenda akarejea Uhispania kujiunga na klabu yake ya zamani Athletic Bilbao mwisho wa msimu huu kandarasi yake itakapomalizika.(El Correo, via Sun)
West Ham nayo inajiandaa kutangaza ofa ya mlinzi wake Declan Rice,19,- ambaye anakibali cha kuchezea mataifa ya Jamhuri ya Ireland na England - kwa kandarasi iliyo imarishwa ya karibu Euro 21,000 kwa wiki. (Football London)
Kutoka BBC
0 COMMENTS:
Post a Comment