October 25, 2018

ALIYEKUWA kocha msaidizi wa Simba, Masoud Djuma raia wa Burundi wikiendi iliyopita alianza majukumu yake mapya ya kuinoa A.S Kigali ya Rwanda akiwa kama kocha mkuu. 


Djuma alianza kuinoa A.S Kigali aliyoingia nayo mkataba wa mwaka mmoja katika mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu ya Rwanda dhidi ya Musanze ambapo kocha huyo alikaribishwa kwenye ligi hiyo kwa kuambulia sare ya bao 1-1. 


Baada ya matokeo ya mechi hiyo ambayo ilipigwa katika Uwanja wa Nyamirambo, A.S Kigali imejikuta ikishika nafasi ya tano katika msimamo wa ligi hiyo inayoshirikisha timu 16 ikiwa na pointi moja. Djuma ataiongoza timu hiyo keshokutwa Jumamosi watakapokutana na Kirehe.

 Kabla ya kutua A.S Kigali, Djuma alikuwa kocha msaidizi Simba ambapo alikatishiwa hivi karibuni mkataba wake baada ya kushindwa kuelewana na kocha mkuu, Patrick Aussems. 

1 COMMENTS:

  1. Daaah Ndugu Mwandishi...
    Huyu kocha alipokuwa bongo kila siku ulikuwa ukimwandama.. hadi ukachangia kumtibulia ajira yake..
    Kaenda zake Chigali bado tu upo nyuma yake... Utakufa!

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic