KOCHA mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera amesema kuwa mchezo wake wa leo dhidi ya KMC ni muhimu kwa washambuliaji wake kuhakikisha wanawafunga mapema ili kukamilisha hesabu.
Yanga ambayo imekuwa na mwanzo mzuri kwenye duru la kwanza, baada ya kucheza michezo saba bila kupoteza hata mmoja huku wakitoa sare mchezo mmoja na kujikusanyia pointi 19.
Zahera alisema kuwa kitu kikubwa ambacho anawasisitizia wachezaji wake ni utulivu wakiwa ndani ya uwanja na kuhakikisha wanapata ushindi mapema.
"Wachezaji nimewaambia ndani ya dakika kumi nahitaji kupata matokeo mazuri ili kuleta ushindani, ligi sio nyepesi kwa kuwa kila timu imejipanga kushinda mchezaji mvivu sitakuwa na subira naye ndani ya uwanja," alisema.
0 COMMENTS:
Post a Comment