October 20, 2018




Waliomteka Mohammed Dewji walitaka fedha na imeelezwa hiyo ndiyo ilikuwa nia yao. Dewji tayari amepatikana baada ya kuachiwa na watekaji hao.


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amesema watekaji hao walikuwa wakimuuliza Mo Dewji kuhusiana na masuala ya fedha, naye akawaambia wampigie baba yake mzazi ingawa hawakufanya hivyo.



"Mo amesema watekaji hao walitaka fedha. Hata hivyo yeye aliwasisitiza kumpigia baba yake kwa kuwa yeye alikuwa nao pale," alisema.

Mo amerejea nyumba ikiwa ni siku ya tisa baada ya kutekwa na watu wasiojulikana Alhamis Oktoba 11 katika Hoteli ya Colessium iliyopo Masaki jijini Dar es salaam.


Ameungana na familia yake akiwa salama baada ya kupatikana usiku wa kuamkia leo kutokana na watekaji hao kumuachia wakitumia gari lilelile walilotumia kumteka.

4 COMMENTS:

  1. Nadhani baada ya kutoka picha za gari na taarifa za polisi kuwa dereva na mmiliki wa gari hilo anajulikana na tayari international police Interpol wapo kazini wa nchi husika gari hilo lilipotoka basi dili likawa limejamba kukawa hakuna jinsi ni kumtema tu. Wahusika lichayakudaiwa kuwa wageni lakini lazima watakuwa wana wenyeji wao.

    ReplyDelete
  2. Ahsanteni sana.
    Allah azidi kutulinda dhidi mafatani na azidi kuumbua hila zao

    ReplyDelete
  3. Tunamshukuru Mungu wetu kwa kuzipokea swala na maduwa zetu. Allahu amesema niombeni nikupeni na tulipo muomba ndio akatupa kapatikana mzima na sasa tuendelee kuiombea duwa nchi yetu iongoze kuwa katika amani na amhidi kila aliekuwa mbaya aongoke ili Mungu aibariki nchi yetu

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic