KIBADEN AMWAGA LAANA KUTEKWA KWA MO DEWJI
Mchezaji wa zamani wa Klabu ya Simba na timu ya taifa ya Tanzania, Abdallah Athuman Seif ‘King Kibadeni’ amelaani kwa kitendo cha Mohamed Dewji ‘Dewji’ kutekwa na kusema kinatishia usalama kwa jamii.
Kwa mujibu wa Championi Ijumaa, Kibadeni baada ya taarifa hiyo ya kuthibitishwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, alisema:
“Tunaomba serikali iwachu-kulie hatua kali hao waarifu ambao wamehusika na tukio hilo la Mo Dewji, tuna-omba izidishe usalama zaidi kwa jamii maana kama mtu maarufu na mwenye fedha katekwa, je, watu wa kawaida siwatatekwa sana.”
0 COMMENTS:
Post a Comment