October 12, 2018


Wakati timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars ikitarajiwa kushuka dimbani leo Ijumaa, kocha msaidizi wa timu hiyo, Hemed Suleiman ‘Morocco’ amesema kikosi kipo fiti na tayari kupambana na lengo ni kuondoka na ushindi na kusonga mbele.

Stars ikiongozwa na nahodha Mbwana Samatta anayeichezea Genk, itaivaa na Cape Verde kwenye Uwanja wa Praia kabla ya kurudiana Oktoba 16, mwaka huu jijini Dar.

Akizungumza kutoka Cape Verde, kocha huyo alisema wachezaji wote wako fiti na tayari kwa mchezo zaidi Watanzania wazidi kuwaombea kuweza kupata matokeo mazuri.

“Kila kitu kinakwenda sawa wachezaji wote wako vizuri na leo (jana) Alhamisi walifanya mazoezi kwa pamoja na kama tulivyosema awali ni lazima vijana wapambane tuweze kupata matokeo na kuwa kwenye nafasi nzuri,” alisema.


Mchezo huo utasimamiwa na waamuzi kutoka nchini Mali ambao ni Boubou Traore, Drissa Kamory Niare na Baba Yomboliba.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic