October 13, 2018


Mbunge wa Kigoma Mjini (ACT Wazalendo) na mdau wa soka nchini, Zitto Kabwe, amewatetea wachezaji wa Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, mara baada ya kufungwa na Cape Verde jana usiku.

Kupitia akaunti yake ya Twitter,  Zitto amesema Stars wameumizwa na tukio la kutekwa kwa mfanyabiashara Mohammed Dewji huku akieleza wachezaji hao wasingepewa taarifa za kutekwa kwa mfanyabiashara huyo ambaye pia ni mdau wa michezo.



Mo ambaye ni mwekezaji katika Klabu ya Soka ya Simba akimiliki asilimia 49 ya hisa za klabu hiyo, alitekwa na watu wasiojulikana Alhamisi, Oktoba 11, 2018 ambap0 mpaka sasa bado hajapatikana.

Jana usiku, Taifa Stars ilifungwa kwa bao 3-0 na wenyeji wao Cape Verde kwenye mchezo wa tatu wa kundi L, kuwania kufuzu fainali za AFCON zitakazofanyika mwakani 2019, nchini Cameroon.

Tanzania sasa inashika nafasi ya mwisho kwenye kundi L ikiwa na alama 2 sawa na Lesotho inayoshika nafasi ya tatu ikiwa na alama 2 lakini ina wastani mzuri wa mabao ya kufunga na kufungwa. Uganda wapo kileleni wakifuatiwa na Cape Verde zote zikiwa na alama 4.

Stars watarudiana tena na Cape Verde hivi karibuni kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic