MBELGIJI AWAKATAA WAWILI SIMBA
Kocha wa Simba, Patrick Aussems, amewaangalia wapinzani wake, Yanga na kubaini kila mchezaji anafunga mabao pindi anapopata nafasi hivyo naye ameamua kufanya kitu Msimbazi.
Simba mpaka sasa ipo nafasi ya tano kwenye msimamo wa ligi kuu ambapo kikosi hicho kimefunga mabao nane na zaidi wanaonekana kuwategemea washambuliaji katika kufanya kazi hiyo.
Mbelgiji huyo ameamua kubadili majukumu baada ya kuona anapata shida kupata matokeo ya ushindi katika mechi zake ambapo washambuliaji wake wanamwangusha kwa kukosa nafasi nyingi za wazi na kuifanya klabu hiyo kupata ushindi kwa taabu.
Kikosi cha Simba kimejaza washambuliaji imara na wenye uwezo mkubwa kama Emmanuel Okwi, Meddie Kagere, Adam Salamba na John Bocco lakini kasi yao ya kufunga uwanjani siyo kubwa.
Aussems alisema timu yake inahitaji matokeo lakini washambuliaji wanaotakiwa kutimiza hilo hawafanyi kazi yao inavyotakiwa kwa kukosa nafasi nyingi za wazi katika lango la wapinzani.
“Lazima nifanye mabadiliko ya haraka kwa sababu nikiwategemea washambuliaji ndiyo wanipe matokeo nitakuwa nachelewa na hatimaye itaniwia vigumu kupata matokeo mazuri kwenye mechi zetu.
“Mipango yangu ni kuifanya timu icheze na yeyote aweze kufunga nje ya hao washambuliaji pekee, naamini hii ni njia sahihi zaidi kuliko kuwategemea wao pekee kunipa matokeo,” alisema Aussems.
rudi kwenye 3-5-2 ya Masoud Djuma
ReplyDelete