October 23, 2018


Beki wa Simba Yusuphu Mlipili amesema kuwa kutopata nafasi ya kucheza ndani ya kikosi hicho ni kutokana na wachezaji wengi kuwa bora.

Mlipili msimu uliopita alicheza mechi nyingi akicheza kwa uelewano mkubwa na Erasto Nyoni ,ila kwa msimu huu mambo yamekuwa tofauti.

"Timu yetu ya Simba ina kikosi kipana kwa hiyo naamini muda ukifika wa kucheza nitacheza bado nina nafasi ya kufanya hivyo ,msimu uliopoita nilicheza kuna wenzangu walikuwa benchi," alisema.

Kabla ya kutua kwa Kocha Patrick Aussems, Mlipili alikuwa kati ya wale waliokuwa wakipata nafasi mara kadhaa chini ya Kocha, Pierre Lechantre raia wa Ufaransa.

Hata hivyo, Mlipili ameendelea kuongeza juhudi kuhakikisha siku moja anafanikiwa kupata nafasi.




1 COMMENTS:

  1. Ajipange atacheza tu ila lazima aamue kuwa anataka kucheza la sivyo patamshinda. Kwa mzungu ukiwa unaweza hapanaga figisu utacheza tu.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic