Meneja wa Mshambuliaji kinda wa Serengeti Kelvin John, Mbaki Mutahaba amesema kuwa nyota wa timu ya Cameroon Samuel Eto'o amehusika kumfundisha kijana huyo.
Kelvin ameenda nchini Dernmark jana kwa mujibu wa kocha wa Serengeti, Oscar Milambo kwa ajili ya majaribio katika klabu ya HB Koge yatakayochukua siku 19 ili kuweza kujaribu bahati yake.
"Tulikutana na Eto'o wiki iliyopita na akapata fursa ya kuzungumza na Kelvin, alimsihi sana adumishe nidhamu na kujituma katika kazi ili aweze kufikia mafanikio pamoja na kuwa mvumilivu," alisema.
Eto'o nahodha wa zamani wa Cameroon alikuwa nchini kwa ziara maalum ambayo ilihusisha kujengwa kwa uwanja mdogo wa michezo nchini.
Mkali huyo wa zamani wa FC Barcelona na Chelsea alipata nafasi ya kuwaona wadau mbalimbali wa soka akiwemo Rais Mstaafu, Jakaya Mrisho Kikwete.
0 COMMENTS:
Post a Comment