October 25, 2018


Mabingwa wa kihistoria Yanga wamefanikiwa kuibuka na ushindi katika mchezo wao wa Saba kwa kuwafunga bao 1-0 KMC, mchezo uliochezwa Uwanja wa Taifa.

Mchezo huo ulikuwa na ushindani kwa timu zote ambapo iliwachukua dakika 89, Yanga kupata bao ambalo lilifungwa na kiungo mkabaji Feisal Abdallah "Fei Toto"  baada ya kupiga faulo ya moja kwa moja iliyomshinda Juma Kaseja.

Ushindi huo unawarejesha Yanga kwenye nafasi ya pili kwa kuishusha timu ya Simba ambayo ina pointi 20 huku Yanga wakiwa na pointi 22, Azam ni vinara wakiwa wamekusanya pointi 24.

KMC wamecheza michezo 11 na wameshinda mchezo mmoja huku saba wametoa sare na wamepoteza michezo mitatu, Yanga wamecheza michezo nane, wameshinda michezo Saba huku wakitoa sare mchezo mmoja.

Mabadiliko kwa KMC DK 73
Omary Ramadhani wa KMC anatoka, anaingia Ramadhani Kiparamoto.

Dk 80,Masoud Abdalla anaingia James Msuva.

Dk ya 89,Ally Ally anapata kadi ya njano.

Mabadiliko kwa Yanga DK 74
Anatoka Thaban Kamusoko anaingia Amissi Tambwe.

3 COMMENTS:

  1. Enter your comment...ongera sana yanga yetu wana kijani na manjano dahaaaaaaaaa jaman mmetupa rah mashabik wenu

    ReplyDelete
  2. Tatizo KMC waliinfia wakiwa na mawazo ya sare au suluhu. Huwezi kucheza ligi kama mtoano, matokeo yake unafungwa bao mwishoni unaadhirika

    ReplyDelete
  3. Walikuwa wafungwe nyingi tu hao, bahati yao!Leo hata Ball possession ilikuwa juu kushinda siku zote.Mdogo mdogo!

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic