LICHA YA KUPEWA DREAMLINER NA SERIKALI, KOCHA STARS AJA NA MTAZAMO TOFAUTI
Baada ya serikali kutangaza kuwa kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' kitapata urahisi wa kuwafunga Cape Verde kutokana na kupatia usafili wa ndege ya moja kwa moja, Kocha Emmanuel Amunike amesema haitakuwa hivyo.
Amunike amesema kuwa mechi hiyo haitakuwa rahisi kulingana na kila timu imejipanga kwa ajili ya kuhakikisha inapata alama ili kupigania tiketi ya kufuzu kuelekea AFCON mwaka 2019.
Amunike ameeleza hayo mara baada ya Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Harrison Mwakyembe, kusema kuwa kitendo cha serikali kutoa ndege 'Dream-liner' ili kuipelekea Stars moja kwa moja mpaka Cape Verde itarahisisha kupata ushindi.
Kocha huyo anaamini kila timu inapambana kujiweka fiti kuanzia kwenye maandalizi mpaka kwenye mchezo, hivyo hakutakuwa na urahisi wowote ndani ya dakika 90.
Cape Verde ambao ni wenyeji kwenye kipute hicho, watakuwa nyumbani Oktoba 12 kuikaribisha Stars tayari kwa mchezo huo wa kundi L ili kusaka tiketi hiyo.
0 COMMENTS:
Post a Comment