MAMBO YAGEUKA KWA ZIDANE KUTUA UNITED: TETESI ZA SOKA ULAYA LEO JUMATATU HIZI HAPA
Agenti wa Zinedine Zidane,46, Kocha wa zamani wa Real Madrid, ambaye amehusishwa na Manchester United huenda asiiongoze klabu hiyo katika ligi kuu ya England.(Marca)
Paul Pogba iliisaidia Man utd kupata ushidi wa kusisimua wa mabao 3-2 wa dhidi ya Newcastle baada ya Jose Mourinho kumshauri kuhusu mbinu za mchezo huo wakati wa muda wa mapumziko. (Sun)
Mshambuliaji wa zamani wa Arsenal anapigiwa upato kuwa meneja wa Aston Villa huku John Terry,37, akitarajiwa kuwa masaidizi wake.(Express and Star)
Arsenal huenda ikamsajili mshambuliaji wa Paraguay Miguel Almiron mwezi Januari mwakani. Mchezaji huyo wa miaka 24 ameifunga mabao 12 mwaka huu kwa MLS Atlanta United.
Ataihama klabu hiyo kwa kima cha Euro milioni 15 mwisho wa msimu huu utakao kamilika mwezi Desemba.(Daily Mirror)
West Brom itarejea na ofa nyingine kwa Bradley Dack wa Blackburn mwezi Januari msimu wa uhamisho wa wachezaji baada ya juhudi zao za kumchukua kugonga mwamba kiungo huyo wa kati wa miaka 24 msimu wa joto. (Birmingham Mail)
Mshambulizi Manolo Gabbiadini amekiri kuwa angelitafakari ofa alizopata msimu wa jota laiti angelijua ataendelea kusalia Southampton.
Mchezaji alianza kucheza katika ligi ya Premier msimu huu siku ya jumapili lakini akatolewa uwanjani baada ya kushindwa na Chelsea mabao 3-0.
Meneja wa Chelsea Maurizio Sarri ame dokeza kuwa Ruben Loftus-Cheek aliachwa nje ya kikosi cha Southampton kwa sababu kiungo huyo alicheza dakika 70 siku ya Alhamisi.
England na Tottenham zina hofu kuhusiana na hali ya Danny Rose baada ya auricio Pochettino kuthibitisha kuwa mchezaji huyo wa miaka 28 anakabiliwa na tatizo la mara kwa mara la kinena (London Evening Standard)
Meneja wa Crystal Palace Roy Hodgson anasema hakuna miujiza itakayobadilisha mkondo wa mchezo wao baada ya kushindwa mara tatu katika mechi nne katika uga wa Selhurst Park (Football London)
Kutoka BBC
0 COMMENTS:
Post a Comment