October 8, 2018


Habari za ndani toka Machester United zinasema kocha Jose Mourinho atatimuliwa kazi kwenye mapumziko haya ya mwishoni mwa juma kama timu yake itapata matokeo mabaya dhidi ya Newcastle United ( Daily Mirror)

Mshambuliaji nyota wa klabu ya Paris St-Germain na timu ya taifa ya Brazil Neymar amefanya mazungumzo na kiungo wa Manchester United Paul Pogba kumshawishi kujiunga na mabingwa hao wa League 1 baada ya kutokua na mustakabali mzuri wa baadae kwa kiungo huyu mwenye miaka 25. (Goal)


Kocha wa Crystal Palace Roy Hodgson amesema timu yake inaweza kumsajili kiungo wa Chelsea Roben Loftus-Cheek,ambaye alicheza kwa mkopo kwenye timu hiyo msimu uliopita (Talksport)

Timu ya Arsenal itamsajili kiungo raia wa Paraguay mwenye umri wa miaka 24 anaichezea timu ya Atlanta United Miguel Almiron,Hayo yamesema na Rais wa timu hiyo ya Marekani Darren Eales (Fox Deportes USA, in Spain)

Kiungo wa Chelsea na timu ya Taifa ya Hispania Cesc Fabregas 31,anatarajiwa kupewa mkataba mpya na Blues kwa sababu mkataba wake unatarajia kuisha mwishoni mwa msimu huu kwenye majira ya kiangazi (Guardian)


Mlinzi wa kati wa timu ya Chelsea na England Gary Cahill ,32, amesema anajianda kukaa kwenye timu hiyo ya Stamford Bridge hadi mwishoni mwa msimu huu ingawa kulikuwa na taarifa zikisema alikuwa na mpango wa kuondoka kwenye timu hiyo wakati wa dirisha dogo la uhamisho mwezi Januari (Evening Standard).

Kutoka BBC

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic