October 8, 2018


Kipa namba wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Aishi Manula, anaamini ubora alionao Kocha Mkuu, Emmanuel Amunike utaisaidia timu kufuzu fainali za AFCON 2019, imeelezwa.

Taarifa imeeleza kuwa Manula ambaye ni sehemu ya wachezaji walioitwa katika kikosi cha Stars amesema kuwa anamwani Amunike kuwa ataiwezesha Stars kufanya maajabu ya kufuzu kuelekea mashindano hayo.

Kipa huyo ambaye amekuwa tegemeo ndani ya kikosi chake cha klabu ya Simba, amefunguka hayo wakati Stars ikiwa kambini kujiandaa na mechi dhidi ya Cape Verde.

Stars itakuwa na kibarua kigumu ugenini dhidi ya Cape Verde, mechi ikipigwa Oktoba 12 tayari kusaka tiketi ya kucheza AFCON mwakani.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic