October 8, 2018


Uongozi wa klabu ya Yanga umeibuka na kufunguka juu ya jezi zake kuwa zaidi ya moja jambo ambalo lilipelekea mashabiki na wadau kuanza kuhoji.

Kwa mujibu wa Kaimu Katibu Mkuu wa klabu, Omar Kaya, ameeleza kuwa wao wameamua kufanya hivyo kwasababu wamependa.

Kaya amesema hakuna mtu wa kuwashinikiza kufanya maamuzi hayo ya kuwa na jezi kwani ni jukumu lao kupanga.

Hatua hiyo imekuja mara baada ya Yanga kuonekana siku kadhaa zilizopita ikiwa na jezi za aina mbili za mazoezi na kuchezea mechi.

Kaya amesema waliamua kufanya hivyo na hakuna mtu yoyote atakayeweza kuwapangia mambo yao maana walikuwa na sababu zao.

1 COMMENTS:

  1. majibu mepesi sana kwenye team kubwa Yanga, huyu ndie aliesema kuwa kocha mkuu hana umuhimu wa kuwepo benchi; that time Zahera hana kibali.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic