October 7, 2018


Straika mwenye asisti za kumwaga ndani ya Yanga, Ibrahim Ajibu amewa­sisitiza mashabiki wa klabu hiyo kuwaunga mkono kama ilivyokuwa kwenye mechi na Simba lakini yeye atapambana kibabe zaidi.

“Kwa sasa Yanga ndiyo nyumbani kwetu kwa hiyo nataka kuona msimu huu tunafanya vizuri lakini pia kuendeleza rekodi yetu ya kutofungwa ambayo tunaishika mpaka sasa.

“Lakini pia niwaombe tu Wanayanga wote kuwa kitu kimoja kuanzia sasa na wasiruhusu mgogoro wowote ule ambao unaweza kukwamisha malengo yetu hayo,” alisema Ajibu na kuongeza kuwa Mbao analala kilaini leo Uwanja wa Taifa.

KIKAO NYUMBANI

Athumani Ajibu ambaye ni kaka mkubwa wa Ibrahim Ajibu amesema kuwa wameamua kukaa chini na mchezaji huyo ili aweze kutambua thamani yake akiwa uwanjani na nje ya uwanja kwa kuwa anapaswa afanye mambo makubwa zaidi ya aliyoyafanya.

“Unajua msimu uliopita Ajibu hakuwa katika ubora wake hivyo tulichoamua kufanya msimu huu tulikaa naye chini na tukamwambia kwamba athamini kazi yake ya mpira kwa kutumia vema kipaji chake alichopewa na Mungu.

“Bado hatujaridhishwa na kiwango anachoonesha kwa kuwa tunatambua ana kipaji kikubwa hivyo kwa kuwa ametusikiliza na ametuahidi atabadilika hivyo tunaamini tutashuhudia makubwa msimu huu,” alisema Athumani.

3 COMMENTS:

  1. Hana lolote alisema mechi ya Simba itakuwa nyepesi mno lakini tuliona alivyotoa ulimi .Hana kitu.

    ReplyDelete
  2. Enter your comment...Sisi mashabiki tunatambua uwezo na mchango wako ndani ya Yanga Wala usikatishwe tamaa na kelele za wapitanjia

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic