Kiungo Haruna Niyonzima ameonyesha kuwa sasa yuko fiti kweli baada ya kuwa kivutio kwa mashabiki waliohudhuria mazoezi ya Simba kwenye Uwanja wa Bocco Veterani jijini Dar es Salaam.
Mabingwa wa soka Tanzania Bara, Simba leo wamefanya mazoezi yao ya mwisho kabla ya kuwavaa Alliance kutoka Mwanza, kesho.
Katika mazoezi hayo, Niyonzima alikuwa kivutio kwa mashabiki waliojitokeza kutokana na aina ya uchezaji wake huku akipangua na kutoa pasi safi.
Hali hiyo ilifanya baadhi kumpigia makofi ya kumpongeza na kuanza kuamini kuwa sasa, Simba wamekamilika katika kiungo.
Kiungo mkabaji wa Simba, Jonas Mkude aliyekuwa majeruhi, naye alionyesha amerejea kazini vizuri baada ya kufanya mazoezi vizuri.
Simba watakuwa na kibarua hicho dhidi ya Alliance kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam na leo walionekana wako tayari.
Kikosi hicho chini ya Mbelgiji, Patrick Aussems kilifanya mazoezi yake kikionyesha ndani yake kuna ari.
0 COMMENTS:
Post a Comment