NOEL MWANDILA AACHIWA MAAGIZO HAYA NA ZAHERA
Wakati kikosi cha Yanga kikiwa kinajiandaa na mchezo wa ligi dhidi ya Mbao FC keshokutwa Jumapili, Kocha Mkuu wa Yanga, Mkongomani, Mwinyi Zahera, amemuachia maagizo Noel Mwandila ya kuhakikisha anashinda mechi hiyo.
Zahera hayupo nchini baada ya kusaifiri kuelekea kwao Congo kutimiza majukumu ya kukinoa kikosi cha timu ya taifa kuelekea mechi za kufuzu AFCON 2019.
Kocha huyo amemtaka Mwandila kuhakikisha anakipanga kikosi vema ili kupata alama tatu dhidi ya Mbao ambao waliilaza Simba kwa bao 1-0 jijini Mwanza.
Agizo hilo ameliacha kwa Mwandila ili kuzidi kuiweka Yanga kwenye mazingira mazuri ya kuhakikisha inachukua taji la Ligi Kuu Bara kwa msimu wa 2018/19 ambao unashirikisha jumla ya timu 20.
Yanga itakuwa mwenyeji wa mchezo huo kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ambapo mechi hiyo itapigwa majira ya saa 12.
0 COMMENTS:
Post a Comment