October 6, 2018


Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda leo ametangaza kuondoa muda wa kikomo kwa wasanii kupiga mziki kwenye matamasha hadi saa sita usiku na sasa amewaongezea muda hadi Saa nane usiku kwa siku za wikiendi pekee.

Hatua hiyo imepokelewa kwa shangwe na wasanii nchini ambao kilio chao kilikuwa kuongezewa muda wa kufanya matamasha ili waweze kujipatia kipato cha kujikimu kimaisha kuendana na kaulimbiu ya Rais wao Mpendwa Dkt. John Magufuli inayowataka watu kufanya kazi.

Hii pia ni matokeo ya kuimarika kwa ulinzi na usalama wa jiji hilo la kibiashara ambapo lengo la RC Makonda ni kuona siku moja watu wanafanya shughuli za kibiashara kwa Saa 24.


Shangwe nyingine Makonda baada ya kupewa nafasi na kueleza jinsi alivyokuwa mlezi wa WCB na kumtaka Diamond aoe kabla mwaka haujaisha. “Leo hii Diamond akimtaka hata mwanamke wa aina gani atampata kwa sababu ana kipaji.

Kuna mstahiki Meya hapa (Benjamini Sitta) nimemwambia mwaka huu ukiisha asipooa namfunga, kuna mwingine naye anaitwa Majizzo yeye juzi kaniwahi kamvisha pete Lulu (Elizabeth Michael).

“Lakini nilikuwa najiuliza huyu naye (Diamond) tumtie ndani au tufanyeje? Lakini nimegundua kwa kazi aliyonayo, Diamond nampa miaka acha kwanza aendelee kuwa sukari ya mioyo ya watu, namtaka baadaye awe zaidi ya kina 50 Cent na Jay Z si mnaona hata Jay Z alifanya muziki akaweka mambo yake.

2 COMMENTS:

  1. Makonda ni mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam na tamko hili linahusu mkoa wake tu....mwandishi uchwara amelielezea tamko la Makonda kama ni la nchi nzima,waandishi wa blog hii ni shida sana

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic