October 23, 2018


Ofisa habari wa timu ya Simba Haji Manara amesema kuwa hawana tatizo na timu ambayo itakuwa inahitaji kumchukua mchezaji yoyote ndani ya kikosi  endapo watafuata utaratibu.

Manara ameyasema hayo baada ya nyota wa timu ya Simba Emanuel Okwi na Shiza Kichuya kuhusishwa na kujiunga na moja ya timu inayoshiriki ligi kuu nchini Ubelgiji ambako Mbwana Samatta anachezea timu ya KRC Genk.

"Hakuna klabu ambayo inaweza kumzuia mchezaji kuitumikia timu ambayo anahitajika,hivyo kwetu sisi mchezaji yoyote tunampa ruhusa kujiunga na timu yoyote ambayo itafuata utaratibu wa kumsajili," alisema.

Kwa sasa wachezaji hao wawili ni sehemu ya wachezaji tegemeo wa Simba ambao ndio mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara.

Kichuya amekuwa akitokea kulia wakati Okwi ambaye ni Mganda, mahiri zaidi anapotokea kushoto.

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic