October 20, 2018





Waziri wa Mazingira, Januari Makamba amekuwa mtu wa kwanza kuzungumza na Mfanyabiashara Mohamed Dewji baada ya kupatikana kwake.



Makamba alisema kupitia mtandao wake wa Twitter, amethibitisha kupatikana kwa Mo na kusema kuwa Mfanyabiashara huyo alitupwa maeneo ya Gymkhana huku akiwa na alama za kufungwa kamba mikononi.


“Nimemuona na kuongea kwa kirefu na Mohammed Dewji. Ni mzima wa afya isipokuwa ana alama za kufungwa kamba mikononi na miguuni. Mnamo saa nane usiku, watekaji waliamua kumtupa kwenye maeneo ya viwanja vya Gymkana. Naamini Polisi watatoa taarifa za ziada kuhusu kilichojiri,” ameandika Makamba.



Dewji alitekwa Alhamisi ya Oktoba 11, saa 11 Alfajiri akiwa anaingia Gym kwa ajili ya mazoezi katika hoteli maarufu ya Collesium. Tokea siku hiyo, kazi ya kumsaka iliendelea na jana, IGP, Simon Sirro alieleza kwamba wamelijua gari lililotumika kumteka Mo Dewji.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic