July 1, 2018


Timu ya taifa ya Ureno imeungana na Argentina kuyaaga mashindano ya Kombe la Dunia kwa kukubali kichapo cha mabao 2-1 dhidi ya Uruguay.

Ushindi wa Uruguay umetokana na mshambuliaji wake anaiychezea klabu ya PSG kutoka Ufaransa, Edinson Cavani aliyetupia mabao yote mawili kambani.

Bao pekee la Ureno limefungwa na Pepe kwa njia ya kichwa kupitia mpira wa kona.

Matokeo hayo yanawafanya nyota Cristiano Ronaldo na Lionel Messi tuwakose kuanzia michezo ijayo baada ya kuyaaga rasmi mashindano hayo.

Messi na Ronaldo walikuwa wanatazamwa zaidi na wafuasi wao kutokana na ushindani mkubwa pamoja na ushawishi walionao pale wanapohusika katika mashindano yoyote kwa pamoja.

3 COMMENTS:

  1. Naweza kusema moja ya timu wachezaji wake licha ya vipaji lakini uzalendo uliotukuka kwa nchi yao kunako wasukuma kupambana kijihadi basi uruguay ni namba moja. Kama watanzania hasa wanamichezo kuna mengi ya kunifunza kule Urusi.

    ReplyDelete
  2. This is URUGUAY Kwa mara ya kwanza ndio wameruhusu goli kutoka Kwa wareno,huu mziki mpaka fainali japo kombe linaenda Mexico.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic